Mhe Lazaro Nyalandu Aweka Mambo Sawa Baada ya Kuzushiwa Kitu Kilichochafua Hali ya Hewa


Mh Lazaro Nyalangu amefunguka kukanusha taarifa ambazo zilikuwa zinasambaa mitandaoni kwamba ametoa maneno ya kukikejeli Chama Cha Mapinduzi.

Mhe. Nyalandu akiwa na gwanda za CHADEMA

Nyalandu ambaye alikuwa Mbunge wa Singida Kaskazini kabla ya kujiuzulu nafasi hiyo,amesema ujumbe huo mchafu uliosambazwa ulikuwa una lengo la kumchafua na kumtengeneza chuki.

“Kuna UZUSHI unaoenezwa mitandaoni kuhusu kauli zangu. Kila nililolisema limerekodiwa na unaweza kupata clips YouTube. Tukumbuke, IMEANDIKWA: Usimshuhudie jirani yako uongo. SOTE Tujenge jamii yenye kuamini katika haki, ukweli na majadiliano ya wazi kuhusu mustakabadhi wa Taifa,” alisema mwanasiasa huyo huku akiwa wamepost screeshort hiyo hapo chini.


Aliongeza,”Imeandikwa, USIMSINGIZIE jirani yako UONGO. Maneno haya ya kigomvi na mengine ya kuzusha yanayozagaa mitandaoni sijayasema mimi. Unaweza kuangalia video clips YouTube kupata ukweli wa kila,”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad