Mimi ni Mke wa Van Vicker – Wema Sepetu

Mimi ni mke wa Van Vicker – Wema Sepetu
Msanii wa filamu Wema Sepetu amefunguka kuizungumzia filamu yake mpya Day After Death ambayo ameshirikiana na muigizaji mkali kutoka Ghana, Van Vicker.



Filamu hiyo imezinduliwa rasmi weekend iliyopita na kwasasa inapatikana kwenye platform ya mtandaoni iitwayo MP TV kutoka nchini Zambia.

Akiongea na Bongo5 Jumanne hii mbele ya waaandishi wa habari, Wema alisema katika movie hiyo yeye ameigiza kama mke wa muigizaji Van Vicker .

“Mimi ni mke wa Van Vicker kwenye movie ya Day After Death najua nitawaliza sana kama kawaida yangu, lakini pia katika hii movie Van Vicker ni baba ambaye anatoka jeshini baada ya kukaa huko kwa miaka sita, anampenda sana mtoto wetu wa kike lakini muda mfupi mume wangu anaanza kuumwa na hataki kabisa mtoto ajue chochote,” alisema Wema Sepetu.

Malkia huyo amedai filamu hiyo imeandaliwa nchini Ghana chini ya director Van Vicker pamoja na kampuni moja kubwa ya production ya nchini humo.

Alisema kwa sasa movie hiyo inapatikana kupitia  app ya MP TV kwa gharama ya tsh 9000 kwa mwezi mmoja ambapo utapata fursa ya kuangalia movie zote zinazopatikana kwenye app hiyo kwa mwezi mzima.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad