''Mkamateni Huyu ni Tapeli na Jizi'' - Mbarawa


Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa, amesema serikali haitasita kuwachukulia hatua wale wote watakaohusika kukwamisha miradi ya maendeleo kwa wananchi na kuwafikisha katika vyombo vya dola, akianza na mkandarasi aliyekwamisha mradi wa Ntomoko.


Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa wa tatu kutoka kushoto.

Mbarawa amesema hayo alipokuwa akikagua mradi wa maji wa Ntomoko uliopo wilayani Kondoa mkoani Dodoma, unaohusishwa na ufisadi wa zaidi ya shilingi bilioni 2.1 gharama ambazo amelipwa mkandarasi wa mradi huo.

“Gharama za mradi zilikuwa ni shilingi bilioni 3 na tukamlipa mkandarasi bilioni 2.1, lakini matokeo yake amekuwa tapeli na jizi sio na anatakiwa kukamata yeye na hata wale tuliowapa dhamana za kusimamia mradi huu.” amesema Mbalawa.

“Tumefanya uchunguzi na sasahivi tutampeleka panapo stahili. Hatuwezi kuona serikali inatoa pesa kwaajili ya maendeleo ya wananchi lakini wajanja, mafisadi wanachukua pesa hiyo kwa maslahi yao binafsi.” Ameongeza.

Mradi huo ambao haujakamilika ulianza kutekelezwa mwaka 2014 kwa gharama ya shilingi bilioni 3 na utasaidia zaidi ya vijiji kumi vya wilaya za Kondoa na Chemba.

Rais Magufuli akiwa katika ziara yake mapema mwaka huu, alitilia shaka mradi huo na kuagiza vyombo vya dola kufanya uchunguzi na wahusika watakaobainika kuhujumu wafikishwe kwenye mkono wa sheria.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad