Melania Trump ameanza ziara ya siku tano barani Afrika, inayolenga kuhamasisha maisha bora kwa watoto katika bara la Afrika.
Mke wa Rais wa Marekani, Melania Trump ameanza ziara ya siku tano barani Afrika, inayolenga kuhamasisha maisha bora kwa watoto.
Ziara yake ilianzia nchini Ghana alikowasili jana Jumanne na kutembelea hospitali ya mkoa. Katika Hospitali hiyo alishuhudia watoto wakipimwa uzito, na kupewa matone ya vitamini.
Bi Trump vile vile alikizuru kitengo cha hospitali hiyo cha watoto waliozaliwa kabla ya wakati. Akiwa mjini Accra, Melania Trump alipokelewa kwa mazungumzo na mke wa rais wa nchi hiyo Rebecca Akufo-Ado na wakabadilishana zawadi.
Ziara hiyo ya Melania, ya kwanza barani Afrika kama mke wa rais wa Marekani, itamfikisha pia katika nchi za Malawi, Kenya na Misri.