WAZIRI wa Kilimo, Dk. Charles Tizeba, ametengua uteuzi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania, Miraji Kipande.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano ya serikali cha Wizara hiyo, Dk. Tizeba ametengua uteuzi wa Kipande kuanzia juzi.
Aidha, Dk. Tizeba amemrejesha Kipande katika nafasi ya awali aliyokuwepo kabla ya kuteuliwa kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa bodi ya Sukari Tanzania.