Mkuu wa Mkoa wa Iringa azuia milioni 70

Mkuu wa Mkoa wa Iringa  azuia milioni 70
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi ameagiza kuchukuliwa kwa sampuli za matofali ya zege 24,082 kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na wakala wa barabara Tanzania TANROADS Mkoa wa Iringa kwa kile alichokidai kuna ubadhirifu katika moja ya miradi ya maji ya kata ya Pawaga

Hapi amefanya maamuzi hayo baada ya kupokea taarifa ya mradi huo kutoka kwa tume maalum aliyoiunda mwezi septemba mwaka huu ili kuchunguza mradi huo wa maji ambao unagharimu shilingi bilionin 4.8.

Hapi amesema “nimeagiza kuchukuliwa sampuli za matofali hayo ya zege yapatayo 24,082 na kupimwa maabara ya wakala wa barabara TANROADS Mkoa wa Iringa kuona kama yanakidhi ubora, na ikibainika kuwa hayakidhi Mkandarasi atalazimika kutengeneza mapya kwa gharama zake mwenyewe.”

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa ameagiza Mkurugenzi wa halmashauri ya Iringa kutofanya malipo yoyote kabla ya kujiridhisha kama hati ya dhamana iliyowekwa na mkandarasi ni halali na inatambuliwa na benki husika ambapo tayari mkandarasi huyo ameshaomba milioni 700.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad