Taarifa za kutoweka kwa mwanahabari wa Saudi Arabia, Jamal Khashoggi na madai ya kwamba huenda ameuawa zimeendelea kugonga vichwa vya habari kote duniani
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres sasa anasema kuwa ''anataka ukweli'' kuhusiana na kutoweka kwa mwanahabari Jamal Khashoggi.
Bwana Guterres ameimbia BBC kuwa anahofia visa vya kutoweka kwa watu kama vile mwanahabari Jamal Khashoggi huenda ikawa "Jambo la kawaida''.
Khashoggi, ambaye amekuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya Saudi Arabia alitoweka Oktoba 2 katika mazingira ya kutatanisha baada ya kutembelea ubalozi wa nchi hiyo mjini Istanbul, Uturuki.
Mwanamfalme Mohammed bin Salman amekosolewa kuhusiana na kutoweka kwa mwanahabari Jamal Khashoggi
Saudi Arabia imekanusha madai kwamba ilitoa amri ya kuawa kwa mwanahabari ikisema madai hayo ni ya "uwongo".
Waziri wa uslama wa kitaifa ya wa Saudi Arabia, mwana mfalme Abdulaziz bin Saud bin Naif bin Abdulaziz, amenukuliwa na shirika la habari la Saudia akisema kuwa ufalme huo pia unataka kubaini ukweli kuhusiana na kisa cha kutoweka kwa mwanahabari Khashoggi.
Vianzo vya habari kutoka idara ya usalama nchi Uturuki vimeiambia BBC kwamba maafisa nchini wana kanda ya sauti na video kuthibitisha kuwa bwana Khashoggi aliuawa ndani ya ubalozi wa Saudi Arabia mjini Istanbul.