Mmiliki wa klabu ya Leicester City ahusika kwenye ajali ya helikopita

Mmiliki wa klabu ya Leicester City ahusika kwenye ajali ya helikopita
Helikopita ya mmilki wa klabu ya Leicester City imeanguka eneo la kuegesha magari nje ya uwanja wa klabu hiyo ilipokuwa ikiondoka uwanjani baada ya mechi ya Ligi ya Premier.

Vichai Srivaddhanaprabha alikuwa ndani ya helikopita hiyo siku ya Jumamosi kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa familia yake.

Mtu mmoja ayeshuhudia alisema aliona mchezaji wa Leicester Kasper Schmeichel akikimbia nje ya uwanja kwenda eneo la ajali.

Leicester ilikuwa imetoka sare ya bao 1-1 dhidi ya West Ham kwenye uwanja wa King Power huku mechi ikikamilika saa moja kabla ya helikopita hiyo kupaa kutoka uwanjani.

Walioshuhudia walisema waliiona ndege hiyo ikiondoka uwanjani kabla ya kupoteza mwelekeo huku wengine wakisema kuwa waliona moto mkubwa wakati ilianguka.,

Majogoo wa jiji la Liverpool kuibuka na ushindi
Klabu inasema inawasaidia polisi na huduma za dharura na itatoa taarifa zaidi hivi karibuni.

Chini ya umiliki wa Bw Srivaddhanaprabha, Leicester City ilishida Ligi ya Premier mwaka 2016.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad