Msiwanyonge, Acheni Watubu - Rais


Rais wa Chama cha Wanasheria nchini (TLS), Bi Fatuma Karume, amesema chama hicho hakitasita kupinga sheria kandamizi endapo serikali itashindwa kuzibadilisha kwani nyingi zinakandamiza maadili na haki za kibinadamu.


Akizungumza na www.eatv.tv Bi Karume amewataka mahakama kuondoa hukumu ya kunyongwa, na badala yake mshtakiwa apewe adhabu nyingine na kupatiwa haki ya kutubu.

"kwanini mtu huyu auliwe kwa kunyongwa? Inakuwa hujampa haki zake za msingi kama binadamu, ni muhimu kila binadamu kuwa na haki yake ya msingi ya kuishi. kutubu ni muhimu kwa kila binadamu hata vitabu vya dini vinasema hivyo, pia 'Criminal Justice system Act', yenyewe inaongelea masuala ya kutubu, wapeni haki ya kutubu na muondoe sheria ya kunyongwa", amesema Bi Karume.

"Criminal Justice system Act, sio adhabu tu, kuna vitu vitatu vinavyozungumiwa ndani yake,cha kwanza ni lazima abadilishwe kisaikolojia,kumfundisha kubadilika kutokana na kosa lake, pamoja na kuwaelewesha watu wanaokuwa nje kutokana na kosa lenyewe kwamba ukifanya hivi adhabu yake ni hii", ameongeza.

Akibainisha vipengele kandamizi, Bi Karume amesema takribani vipengele 40 vya sheria zinatakiwa kubadilishwa ambavyo ni pamoja na Newspaper Act,(sheria za magazeti)Witch craft Act, Corporal punishment act (kupigwa viboko), Criminal act (sheria za mauaji) na ile inayowataka ombaomba kukamatwa na kuweka ndani.

"Zipo sheria nyingi ambazo ni kandamizi lakini katika hizo nilizozitaja nyingi zina wakandamiza wahusika, mfano Newspaper Act ilibadilishwa, lakini hii mpya ya sasa imekuwa ni kandamizi zaidi ikiwanyima haki wahusika, hivyo sisi kama TLS lazima tutambue sheria kandamizi na tuzijadili mahakamani,ili zitatuliwe na ikiwezekana zibadilishwe".
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad