Mtatiro aibuka, amjibu vikali Meya wa Ubungo, " Lowasa, Zitto walikosea?"


Alieyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya uongozi Chama Cha Wananchi (CUF) Julius Mtatiro, amesema kuwa hakuna makosa ya kisiasa aliyoyafanya ya kukihama chama hicho na kujiunga CCM, kwa mujibu wa katiba za vyama. 

Katika waraka alioutoa kwenye mitandao ya kijamii ambao umelenga kumjibu Meya wa Manispaa ya Ubungo Boniface Jacob, kufuatia kumkosoa kwa yeye kujiunga na Chama cha CCM na kukihama chama Cha CUF. 

Amesema kuwa, kwa mujibu wa katiba za vyama kipo kipengele kinachohalalisha mtu yoyote ama kiongozi kutoka chama kimoja kujiunga na kingine ambapo amedai endapo Jacob ataendelea kulizungumzia suala hilo ama kumosoa itakua haamini katiba za vyama wanavyovisimamia. 

“ Ikiwa kuhama chama ni makosa basi hamziamini katiba zenu, kaka kujidanganya kuwa ni dhambi mwanasiasa kuhama chama wakati kuna viongozi mbalimbali ikiwemo Zitto alipohama alikosea? Lowassa je? Sumaye? Mahanga? Kubenea? Uhuru Kenyatta?”alihoji Mtatiro. 

Ameendelea, " kuhama chama siyo kufanya makosa ya kisiasa, labda nikueleweshe tu kidogo, Winston Churchil alihama vyama mara tatu kasome niambie, Mchango wake hapa duniani ulivyo mkubwa kama kuhamisha milima. 

Ambapo hata Donald Trump amehama vyama au kubadilisha itikadi mara tano tangu 1987. Rais Buhari wa Nigeria amehama mara nne, Raila Odinga amehama mara sita. 

Nikujulishe pia ya kwamba Marekani, kati ya mwaka 2000 – 2010, zaidi ya maseneta na wabunge 100 wamehama kutoka Republican na kuhamia Democrat (vyama hasimu kabisa, ni kama kutoka CCM kwenda Chadema vice versa).” amesema Mtatiro. 

“Kuhama kwangu CUF msikufanye kisingizio, tatueni matatizo halisi yaliyomo upinzani, mtapata kina Mtatiro wengine wengi wanaozaliwa kwa ajili ya baadae, lakini kuwapoteza kina Mtatiro wa sasa kutakuwa somo kwenu kutotumia siasa za upinzani kama kichaka cha kujifichia”amesema Mtatiro. 
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad