MKALI wa Filamu za Kibongo, Riyama Ally amesema amelazimika kuingia katika gemu la muziki wa Bongo Fleva baada ya mumewe, Haji Mwalimu ‘Leo Mysterio’ kumsukumia huko kwa kumshirikisha ndani ya wimbo wake wa Wanaume wa Dar. Riyama aliiambia Mikito Nusunusu kuwa, yeye si muimbaji kivile lakini linapokuja suala la kumsapoti mume wake, haoni shida kujiingiza huko.
“Sina kipaji cha kuimba, napenda sana kuigiza ila nitakuwa namsapoti mista wangu katika nyimbo zake kama vile kuingiza maneno kuntu,” alisema Riyama. Akaeleza kuwa, wimbo huo umetungwa maalumu kwa ajili ya kuwakumbusha wanaume wasiopenda kufanya kazi na kukaa vijiweni kuinuka na kuacha kuchagua kazi wakati wanategemewa. “Kama ni kijana akisikiliza wimbo huo ambao nami nimeimba, atapata fursa ya kujifunza jambo,” alisema Riyama.