Mungu Mkubwa Hawa Afanyiwa Upasuaji Mkubwa wa Moyo Salama...Babu Tale Afunguka


Kwa mujibu wa Meneja wa Diamond Platnumz, Babu Tale, msanii Hawa aliyeshirikishwa kwenye wimbo wa nitarejea wa Diamond amefangiwa operation ya moyo yenye mafanikio makubwa kwa masaa matano,Tale ameandika kupitia kwenye akaunti yake ya instagram kuwa msanii huyo amezinduka na anaendelea vizuri,mambo yakienda sawa watarejea Dar es salaam baada ya wiki moja.

Hawa alisafirishwa kwenda India kwenye matibabu kwa msaada wa CEO wa wa WCB Chibu Dangote,ambapo safari hiyo pamoja na matibabu yamegharimu shilingi za Kiganzania Milioni 50,awali ilidaiwa kuwa dada huyo anaugua ugonjwa wa ini kutokana na athari za madawa ya kulevya na pombe lakini madaktari nchini India walibaini kuwa ugonjwa unaomsumbua Hawa ni moyo unaopelekea mwili na timbo kujaa maji.

Kwa niaba ya members wote wa Celebrity forum na Jf kwa ujumla,Napenda kumpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Wasafi Media Nasib Abdul kwa moyo wa kufanikisha matibabu ya Hawa🙏.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad