Mwanamuziki Ariana Grande Bado Hayupo Sawa Kutokana na Kifo cha Ex Wake

Scooter Braun Meneja wa Pop staa Ariana Grande amesema mteja wake bado anapambana na mambo magumu kwa sasa ndio maana ameshindwa kufanya show katika tamasha la kuchangisha pesa kwaajili ya wagonjwa wa Saratani.

Ni siku 38 toka amefariki Ex wake Ariana Grande 'Mac Miller' na bado Ariana hajawa sawa kutokana na lawama za dunia kuwa alivyomwacha rapa huyo ndipo akazamia zaidi kwenye matumizi ya dawa za kulevya mpaka kusababisha kifo chake.

Pia TMZ Imeripoti kuwa Ariana Grande na mpenzi wake ambaye walitegemea kuwa wachumba hivi karibuni Pete Davidson wameachana na kufuta mipango yote ya sherehe ya uchumba, May mwaka huu wawili hawa walitangaza hatua hio kwenye maisha yao na Ariana alivalishwa pete yenye thamani ya dola laki moja na Pete, wanasema bado ni marafiki ila mahusiano yao yameisha.
-
Mac Miller alifariki September 7, 2018 kwa kutumia dawaza kulevya kupita kiasi

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad