MWILI wa aliyekuwa mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya Deutsche Welle (DW), Isaac Muyenjwa Gamba umeasili Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, leo Jumatatu alfajiri ndege ya Shirikia la Turkish Airline.
Mtangazaji wa zamani wa Redio Tanzania Dar es Salaam (sasa TBC FM), Ahmed Kipozi (kulia) akisalimiana na Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya Deutsche Welle (DW), Andrea Schmidt, mara baada ya kuwasili kwa mwili wa Isaac Gamba katika Uwanja wa Ndege wa JNIA, usiku wa kuamkia leo.
Watu mbalimbali wamejitokeza Uwanjani hapo kuupokea mwili wa Gamba wakiwemo wanahabari ambao alifanya nao kazi kwenye vituo mbalimbali vya redio na televisheni hapa nchini, Sam Mahela, Zomboko, Adballah Mwaipaya na wengine.
Zomboko akiwa na mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya DW, wakati wa kupokea mwili huo.
Baada ya kupokelewa, mwili huo umepelekwa katika Hospitali ya Jeshi ya Lugalo ambako ibada na shughuli nzima ya kumuaga marehemu zitaanza leo Jumatatu majira ya saa tano asubuhi na baadaye utapelekwa airport tayari kwa safari kuelekea kwao Bunda kupitia Mwanza kwa ajili ya maziko.
Mtangazaji, Adballah Mwaipaya (kulia) wakati wa kupokea mwili huo.
Aidha, wadau wa Mwanza kuanzia saa tano asubuhi kesho katika Viwanja vya Ofisi ya UTPC watapata nafasi ya kumuaga mpendwa Gamba na baadaye msafara wa magari utaondoka kuelekea Bunda kwa mazishi.
Gamba alifariki wiki iliyopita jijini Bonn nchini Ujerumani alikokuwa akifanya kazi Zake.
Mwili wa Issac Gamba Wawasili Dar Kuagwa Leo Lugalo
0
October 29, 2018
Tags