KWA mujibu wa ofisa mmoja wa serikali ya Uturuki asema mwili wa mwanahabari, Jamal Khashoggi, ulicharangwa vipande baada ya kuawa ili kupoteza ushahidi
Khashoggi alionekana akiingia ndani ya Ubalozi wa Saudi Arabia tarehe 2 mwezi huu na hakuonekana tena baada ya kuingia katika jengo hilo la ghorofa sita.
Inaelezwa kuwa watu waliomfanyia mahojiano Jamal na hatimaye kumuua walipewa maagizo na mtoto wa Mfalme wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman.
Mwandishi huyo alijikita katika kufichua maovu ya utawala wa kifalme wa Saudi Arabia kupitia kazi yake ya uandishi wa habari
Habari nyingine zinasema Khashoggi alikuwa anatuhumiwa kuwa na uhusiano na utawala wa Qatar ambao una uhasama na ufalme wa Saudi Arabia.
Wakati watu wengi duniani wakitaka kujua kilichomfika Khashoggi, jana (Jumanne) Rais Trump wa Marekani na Waziri wa Mambo ya Nje, Mike Pompeo, wamesema Saudi Arabia imewajulisha kwamba uchunguzi juu ya tukio hilo umeanza na majibu yatatolewa karibuni.