Mwingine Serengeti Boys apaa Ulaya


Mchezaji wa Serengeti Boys ambaye anakipiga katika klabu ya Singida United, Ally Hamisi Ng’anzi amepata dili la kucheza soka barani Ulaya katika nchi ya Jamhuri ya Czech.


Mchezaji huyo anayecheza nafasi ya kiungo wa kati, amepata nafasi ya kucheza katika klabu ya MFK Vyskov inayoshiriki ligi daraja la pili nchini humo.

Taarifa rasmi iliyotolewa na Mkurugenzi wa klabu ya Singida United, Festo Sanga kupitia ukurasa rasmi wa Istagram imesema, 

“ Kwa niaba ya uongozi wa klabu, tunamtakia safari njema na mafanikio mema mchezaji wetu huyu tukiamini atafika mbali katika safari yake ya mpira”, imesema taarifa hiyo.

“Amepata timu hiyo ikiwa ni jitihada za klabu yetu kuwatafutia wachezaji wakitanzani nafasi ya kucheza soka kwenye timu mbalimbali barani Africa na hata nje ya Africa, hivyo tunaamini kuna wachezaji wengine watapata timu siku si nyingi ”, imeongeza taarifa hiyo.

Ally Ng’anzi anakuwa mchezaji wa pili kupata nafasi ya kwenda kucheza soka barani Ulaya kutoka katika kikosi cha Serengeti Boys, baada ya mapema wiki hii mchezaji, Morice Abraham kwenda nchini Denmark kufanya majaribio.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad