Pia amewataka wasanii wenye nia ya kutaka kutengeneza filamu katika Hifadhi ya Taifa wawasaliane na Uongozi wa Hifadhi za Taifa au wawasiliane na yeye mwenyewe moja kwa moja.
Ametoa rai hiyo wakati akifunga tamasha la utamaduni wa mtanzania inayowakilishwa na jamii za mkoa wa Lindi lililofanyika kwa muda wa siku nne katika kijiji cha Makumbusho jijini Dar es salaam
Aidha, Ameiasa jamii iitumie mitandao ya kijamii kujipatia elimu badala ya kusambaza picha ambazo ni kinyume cha maadili ya Mtanzania.
Ameongeza kuwa Jamii iwakemee wasanii wenye tabia hiyo badala ya kusubilia Serikali ndo ichukue hatua.