Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, ameagiza wanafunzi 682 walioondolewa katika usajili wa chuo Kikuu cha Dar es Salaam kurudishwa.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Oktoba 22, muda mfupi baada kufungua mafunzo ya wahasibu yanayoendelea jijini Dar es Salaam Profesa Ndalichako amesema amesikia suala hilo mwishoni mwa wiki na tayari ameshauagiza uongozi wa Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) na uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kukaa pamoja na kumaliza tofauti hizo.
“Chuo Kikuu kina nafasi 3,000 tatizo lilikuwa ni la kiufundi kutokana na wanafunzi wengi kupenda chuo hicho ,hivyo nimeomba uongozi kumaliza tatizo hilo na watoto waweze kupokelewa.
“Wengi wanapenda UDSM na tatizo lilikuwa linaweza kurekebishika na wote ni idara za serikali, TCU na UDSM hawakutakiwa kushindana na ndiyo maana nimewaagiza hadi Jumamosi wawe wamemaliza tofauti zao nafikiri hadi leo saa tisa watakuwa wameshawekana sawa,” amesema Profesa Ndalichako.
Ndalichako aingilia kati wanafunzi 682 waliofutiwa usajili UDSM
0
October 22, 2018
Tags