Ndalichako Atumbua Vigogo Wawili Wizara ya Elimu

Ndalichako Atumbua Vigogo Wawili Wizara ya Elimu
WAZIRI Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amemwagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kuwaondoa kwenye vyeo vyao Mratibu wa Miradi na Kaimu Mkurugenzi wa Mafunzo ya Ualimu kwa kushindwa kusimamia majukumu yao na kupelekea baadhi ya miradi kushindwa kukamilika kwa wakati.

Aliwataja viongozi ambao wanatakiwa kuondolewa katika nafasi zao na kuondolewa katika Wizara hiyo ni Mratibu wa Miradi Fredrick Shuma na Kaimu Mkurugenzi wa Mafunzo ya Ualimu Basiliana Mrimi.

Profesa Ndalichako alitoa kauli hiyo jana wilayani Nzega wakati akikagua mradi wa upanuzi wa Chuo cha Ualimu Ndala na kukutana miradi hiyo iko katika hali isiyoridhisha. Alisema utekelezaji wa mradi wa upanuzi wa Chuo cha Ualimu cha Ndala hauridhishi na kusababisha kushindikana wanachuo wengi kuanza katika mwaka huu wa masomo.

Profesa Ndalichako alisema watendaji hao ni miongoni mwa waliosababisha vifaa kwa ajili ya vyuo vya ualimu vya sayansi kupelekwa katika vyuo ambavyo havifundishi sayansi na kupelekea baadhi kupitwa na wakati na kusababisha hasara kwa Serikali.

 Aidha Waziri huyo ametoa onyo kwa Mhandisi wa Wizara hiyo George Sambali kwa kushindwa kukagua miradi ya ujenzi inayoendelea hadi wasubiri Waziri na Naibu wake watembelea ndio nao waonekana jambo ambalo linasababisha kujengwa kwa miradi ambayo sio mizuri na inachukua muda mrefu.

Alisema suala la kuhakiki ubora wa miradi ni kazi ya wataalamu na sio kungoja viongozi waendele ndio marekebisho yafanyike jambo linalosababisha baadhi ya miradi kuchelewa. Profesa Ndalichako alimwonya Mkuu wa Chuo cha Ualimu Ndala Abinego Ndikumwe kutopokea majengo yaliyokarabatiwa na United Builders ambayo yameonyeshwa huku yakiwa na mapungufu mengi.

Alisema kabla ya kuyapokea wahakikishe wahusika wamefanyia kazi mapungufu yote na kufikia Mwezi Novemba wakabidhi kazi ikiwa imekamilika. Kuhusu Kampumi ya Unite Builders ambayo inakarabati na kujenga baadhi ya majengo ameitaka kuhakikisha inakabidhi kazi ifikapo Novemba ikiwa katika hali nzuri na kuongeza nje hapo hawatapa kazi yoyote ya Serikali.

Alisema majengo ambayo watajenga lazima yaonyeshe thamani ya bilioni 3.1
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad