Ndumbaro Aanza na Makampuni 41

Ndumbaro aanza na makampuni 41
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Dkt. Damas Ndumbaro ametangaza ujio wa makampuni makubwa 41 ya uwekezaji kutoka nchini Ubelgiji ambayo yamepata mwaliko wa Wizara.

Akiongea leo na wanahabari jijini Dar es salaam, Dkt. Ndumbaro amesema makampuni hayo yatakuwepo nchini kwa siku 4 hadi 5 kwa lengo la kufungua fursa za uwekezaji katika sekta mbalimbali ikiwemo Utalii na Nishati.

"Ushirikiano wetu na Ubelgiji umekuwa mkubwa sasa na kupitia Ubalozi wetu nchini humo umewezesha ujio huu ambapo leo mchana tunawapokea rasmi wangeni hao na tuna imani utafungua ujira mbalimbali zikiwemo za moja kwa moja".

Aidha amebainisha kuwa wageni hao wataingia leo na kuondoka Oktoba 28 ambapo mbali na shughuli mbalimbali watashiriki katika kongamano kubwa la wafanyabiashara katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam ambapo tayari wafanya biashara zaidi ya 200 wa hapa nyumbani wamethibitisha kushiriki.

Kwa upande mwingine Mh. Dumbaro ambaye ni mbunge wa Songea Mjini ameeleza kuwa watanzania wapatao 30 mapema mwaka huu waliokwenda nchini Ubelgiji kushiriki mkutano mkubwa wa kujadili uwekezaji nchini kwenye sekta ya madini na nyinginezo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad