Aliyekuwa Mbunge wa Simanjiro (CHADEMA), James Ole Millya.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeeleza kushtushwa na taarifa za mbunge wake wa Simanjiro mkoani Manyara, James Ole Millya kujiuzulu kwakuwa aliwahi kukanusha tuhuma hizo mwanzo.
leo Oktoba 8, Katibu wa CHADEMA Kanda ya Kaskazini, Aman Golugwa amesema kuwa taarifa hizo ameziona kupitia mitandao ya kijamii na ameshangazwa kwakuwa aliwahi muuliza na alikanusha kwenye mitandao, na kuhusu barua ya jana amejaribu kumtafuta lakini hakuapatikana kwenye simu yake ya mkononi pamoja na watu wake wa karibu.
"Millya mwanzo alikana kwakuandika kwenye mitandao, lakini hii ya jana hajafanya hivyo jambo linalopelekea tuamini kwakuwa barua ile ina sahihi mbichi na ndio sahihi yake”, amesema Golugwa.
Barua aliyoandika Millya kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai jana Oktoba 7, ilidai kuwa amefanya uamuzi huo kutokana na mwenendo wa siasa za upinzani kutokuwa na afya na kupelekea kuchelewesha maendeleo ya wananchi wa jimbo lake. Hata hivyo, Millya hakupatikana kuelezea barua inayosambaa kuwa amejiuzulu kutokana na kuzima simu zake.
Siku chache kabla ya kujiuzulu Millya alinukuliwa akisema kuwa haridhishwi na baadhi ya mambo ndani ya chama chake na kudai kuwa CHADEMA hali si nzuri kwani si rahisi tena kukosoana ndani ya chama.