STAA wa PSG, Neymar, juzi alionyesha kuwa bado anaweza kuonyesha kiwango cha hali ya juu baada ya kuifungia timu yake mabao matatu ‘hat trick’ walipoichapa Red Star Belgrade mabao 6-1 kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Mchezo huu umemfanya Mbrazili huyo kuweka rekodi mbili muhimu kwenye maisha yake ya soka.
Moja; alikuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao mawili ya faulo kwenye mchezo mmoja wa Uefa, kuanzia Cristiano Ronaldo alipofanya hivyo mwaka 2009.
Pia alifikia rekodi ya kuwa mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa wale wazaliwa wa Brazil baada ya kufikisha mabao 30 na kulingana na Ricardo Kaka.
Matokeo haya yanamaanisha mshambuliaji huyo sasa amehusika kwenye mabao 49 katika michezo 49 ya Uefa aliyocheza.