Ni Kwanini Watu Waliopata Division 3 na 4 Sekondari Wana Mafanikio Katika Maisha Kuliko Wale Wenye Division 1 na 2

Najua wengi hamuwezi amini lakini kuna utafiti nimeufanya kwa wale tuliomaliza kidato cha nne kuanzia mwaka 2010 kushuka chini ambapo kipindi hicho mtu ukipata division one au two form four ulikuwa unaheshimika mtaani na ilikuwa ni heshima sana kwa ndugu na majamaa.

Lakini kwa wale waliopata division 3 au 4 wengi walikuwa wanadhalaulika, wanaonekana wamefeli shuleni lakini pia divion 3 na 4 waliofeli, kipindi hicho wazazi ambao watoto wao walionekana watoto wao kufanya vibaya walionekana watoto wao hawana akili kuliko wale watoto zao waliopata divion one waliheshimika mnoo.

Lakini baada ya miaka mingi kupita tukija katika level ya maendeleo na mafanikio serious wengi waliopata division 4 na 3 ndo wenye maendeleo na mafanikio katika maisha siku na ndio wengi kwa sasa wameajiriwa serikalini, sekta binafsi, wafanyabiashara kubwa kubwa ndo hao mafanikio yao tofauti na wenye div 2 na 1

Je, ni kwanini iwee hivyoo wenye akili za kawaida wafanikiwe kuliko wenye akili nyingi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad