Rapper Cardi B ameamua kufunguka mengi kuhusiana na bifu lililokuwa likiendelea kati yake na Nicki Minaj, hii ni baada ya Nicki kuzungumza kwenye radio yake ya ‘Queens Radio’ kuhusu bifu hilo.
Cardi B amegusia ishu ya namba yake ya simu kuvujishwa na kuanza kupokea maneno machafu ambayo yanasadikika kuwa yanatoka kwa baadhi ya mashabiki wa Nicki, Cardi B alisema kuwa aliyevujisha namba yake na namba ya mdogo wake Hennesy ni Nicki na sio mwingine.
Kwenye baadhi ya videos alizopost Cardi B kupitia ukurasa wake wa IG amezungumza na kusema kama Nicki Minaj ni mtu mzima basi wangemaliza tofauti zao kwa kuzungumza na sio kuongelea tofauti zao kwenye vyombo vya habari.
Baada ya videos hizo Nicki Minaj alionekana kumaliza bifu hilo kupitia ukurasa wake wa twitter na kusema kwa sasa tuangalie zaidi vitu vilivyo chanya , sitozungumza kuhusu huu ujinga tena.
“Sawa tuzingatie vitu chanya kwa sasa, wote tumebarikiwa na ninajua kuwa hichi kitu kinafurahisha na kuburudisha watu wengi lakini sitoongelea huu upuuzi tena. Nashukuru kwa ushirikiano na jitihada za kila mwaka, Nawapenda”
Cardi B alipokea ujumbe huo wa Nicki Minaj na kumjibu kwa kusema “basi sawa, tuweke kila kitu chanya na tusukume kila kitu”
Nicki Minaj Atumia Busara Kuzika Bifu Lake na Cardi B
0
October 30, 2018
Tags