Nicki Minaj Kuja na Documentary Iliyojaa Unyanyasaji

Nicki Minaj kuja na Documentary iliyojaa unyanyasaji
Rapper Nicki Minaj ametudokezea ujio wa makala yake ya “Queen Documentary” ambayo itagusia maisha yake ikiwemo unyanyasaji aliowahi kuhushuhudia kutoka kwa baba yake mzazi na kuapa kuwa hatokubali kunyanyaswa na mwanaume.

Kwenye mahojiano aliyoyafanya Rapper huyo na Mtangazaji Lauren JNel amesema kuwa kitu kikubwa ambacho kimemuathiri hadi leo ni unyanyasaji aliowahi kuushuhudia kutoka kwa Baba yake mzazi kumpiga Mama yake hadi kufikia hatua ya kuingilia kati ugomvi wao.

Nicki Minaj ameongezea na kusema kuwa aliwahi kutojiamini tena kwa sababu tu ya Mtu mmoja ambaye alitaka kumshusha chini kutokana na unyanyasaji alioupata hadi kumpelekea  kushindwa kuingia studio kuendelea kufanya kazi zake za muziki.

“Mama yangu alikubali kumuachia Baba yangu amfanyie fujo na nilikua nikiamua ugomvi wao lakini tokea hapo niliapa kuwa hakuna Mwanaume ambaye ataninyanyasa  au kunifanyia fujo”

“Ilifikia wakati sikujitambua tena kwa sababu ya Mtu mmoja ambaye alinifanya nijiskie niko chini, niliogopa hadi kwenda studio mara ghafla nilipokuwa Miami nilipata mzuka baada tu ya kubadilisha mazingira na nikarudi studio za New York” –Nicki Minaj

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad