Nilipokutana na Diamond Platnumz ana kwa ana tukaongea

Ni shabiki wake sana, japo nampenda zaidi Dully Sykes. Jamaa nilimuona Posta mwezi huu mwanzoni, nikamwita "Simbaa". Hakuitika nikamwita tena akiwa mbali hakuskia ila kuna kabaunsa kakamgusa akanigeukia nkampungia mkono akanipungia mkono na kuzungusha mkono kuwa anakuja.

Sasa nikajiambia haka kajamaa kaongo kanataka kiki ya kujifanya mtu wa watu. Nikaendelea na yangu, dakika kumi karudi kanisalimu akanipa elfu kumi na alikuwa mstaarabu sana.

Akakaa kwenye bao gumu na kunisalimia, akanishukuru kwa sapoti. Huyu dogo sio mchawi ni mnyenyekevu kutokana na maisha magumu yeye na mamake waliyopitia.

Nimejifunza mengi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad