Nyota Serengeti Boys Aula Denmark


NYOTA aliyeng’ara katika kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys kilichoshiriki michuani ya kufuzu kwa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Maurice Michael anatarajiwa kuondoka nchini Oktoba 8, mwaka huu kwenda Denmark kujiunga na klabu ya FC Midtjylland ya Ligi Kuu ya huko. 

Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Kocha wa Serengeti Boys, Oscar Milambo amesema kuwa hiyo ni sehemu ya mpango wao wa kuwapeleka wachezaji wa timu hiyo kujiunga na klabu mbalimbali Ulaya kucheza soka la kulipwa. 

Mbali na Michael, wengine saba waliopo kwenye mpango wa kupelekwa Ulaya hivi karibuni ni Kelvin John, Bernard Pastory, Agiri Ngoda, Edson Mshirakandi, Salum Milinge, Pascal Msindo na Alphonce Mabula ambao wote waling’ara kwenye michauno ya CECAFA AFCON Qulifyng Agosti mwaka huu, Tanzania ikiambulia nafasi ya pili baada ya kufungwa na Uganda kwenye fainali. 

Na hatua hiyo inakuja wakati Serengeti Boys ikiwa inajiandaa kwa michuano ya AFCON U17 itakayofanyika Mei mwakani mjini Dar es Salaam. 

“Michael ndiye atakuwa mchezaji wa kwanza kuondoka huku wachezaji wengine saba wakifuatia baadae, mazungumzo na klabu za barani Ulaya yanaendelea na tumefikia sehemu nzuri. Huu ni mpango maalumu wa kuhakikisha tunakuwa na wachezaji wengi wanaocheza nje, ambao watakuja kuwa msaada mkubwa hapo baadaye,”amesema Milambo. 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad