Nyota wawili wa Azam FC wakosekana miezi miwili

Nyota wawili wa Azam FC wakosekana miezi miwili
Wachezaji wawili wa klabu ya soka ya Azam FC, kiungo Frank Domayo na mshambuliaji Paul Peter, watakosekana uwanjani kwa takribani miezi miwili, baada ya kugundulika kuwa na matatizo ya goti kila mmoja wakiumia kwa nyakati tofauti.



Kwa mujibu wa msemaji wa klabu hiyo Jaffar Idd, nyota hao wawili watapata matibabu kwa njia tofauti baada ya kupata vipimo nchini Afrika ya kusini.

Jaffar amesema kwa mujibu wa madaktari, Paul Peter amelazimika kubaki nchini Afrika kusini kwaajili ya kufanyiwa upasuaji kutokana na tatizo lake kuwa kubwa na matibabu yake kuhitaji upasuaji tofauti na Domayo ambaye atatibiwa kawaida tu.


''Domayo tumempokea jana Oktoba 15, 2018, kutoka Afrika Kusini na ambapo ripoti ya daktari inasema kuwa hatafanyiwa upasuaji na badala yake atatibiwa hapahapa nchini ila Peter atafanywa upasuaji'', amesema.

Jaffar ameongeza kuwa wanatambua mchango wa wachezaji hao ndani ya kikosi chao na wanawaombea wapone haraka ili warudi kwenye timu kwaajili ya kuendelea na majukumu yao.




Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad