Nyumba Mpya ya Diamond Nayo Yakumbwa na Utata.



Ikiwa jana October 2 msanii wa muziki wa bongo fleva DIAMOND  alikuwa akisherekea kumbukumbu ya sikukuu ya kuzaliwa, na alitimiza ahadi aliyowahi kutoa hapo nyuma kwamba siku hiyo ataonyesha mjengo wake mpya kwa mara ya kwanza.

Na kweli swala hilo lilitimia baada ya Diamond kuonyesha mjengo huo kwa mara ya kwanza na kuibua hisia kubwa kwa mashabiki na watu wake wa karibu,  lakini nyumba hiyo imezua utata tena baada ya kusemekana kuwa nyumba hiyo sio ya kwake na kwamba amepanga tu.

Skendo hizo zinzkuwa nyingi kwa Diamond katika kila nyumba anayonunua, ikianza ile ya afrika ya kusini, ikaja studio ya wasafi na nyumba ya Hamisa Mobeto lakini sasa hivi tena ni hii mpya anayosema kuwa ni ya kwake mwenyewe.

Hata hivyo Diamond amekuwa kimya katika kila tukio la aina hii  na inawezekana hii yote ni kwa sababu ukweli anaujua mwenyewe.

Hata hivyo baada ya kufatilia sana ilikuja kuonekana kuwa nyumba hiyo ilikuwa ikiuzwa na imenunuliwa kwa shilingi bilion 2, hivyo waliokuwa wakisema kuwa sio mjengo wake walifumbwa midomo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad