Polisi Yafunguka Kuhusu Agizo la Waziri Lugola la Kutoa Dhamana Hadi Wikiendi "Tutaendelea Kutoa Dhamana kwa Kufuata Utaratibu wa Sheria"

Polisi Wafunguka Kuhusu Agizo la Waziri Lugola la Kutoa Dhamana Hadi Wikiendi "Tutaendelea Kutoa Dhamana kwa Kufuata Utaratibu wa Sheria"
Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola, ametoa agizo kwa jeshi la polisi nchini kuhakikisha dhamana kwa watuhumiwa inatolewa kwa saa 24 katika siku zote 7 za wiki, tofauti na zamani ambapo ilikuwa inatoka mwisho ijumaa jioni.



Lugola alitoa agizo hilo wikiendi iliyopita wakati akiongea katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Basanza wilayani Uvinza, Mkoani Kigoma, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi mkoani humo.

“Hii tabia sijui imetoka wapi ambayo imejengeka kwa baadhi ya askari polisi, eti mtu akiingia mahabusu ya polisi siku ya Ijumaa ikifika siku ya Jumamosi na Jumapili hawatoi dhamana wakisema dhamana mpaka Jumatatu, hii tabia sio sahihi na ife haraka iwezekananavyo.” Alisema Waziri Lugola.

Jeshi la Polisi kupitia kwa msemaji wake Barnabas Mwakalukwa, limeeleza kuwa wao kama jeshi la polisi wataendelea kutoa dhamana kwa kufuata utaratibu wa sheria.

''Dhamana ni haki ya kila mtuhumiwa pia ni bure, sisi tunafanya kazi kwa mujibu wa sheria na utawala bora, ila kuna makosa yanayoweza kutolewa dhamana na mengine hayaruhusu dhamana lakini mtuhumiwa pia anawajibu wa kutimiza masharti ya dhamana'' amesema Mwakalukwa.

Aidha Mwakalukwa amesema kwasababu suala hilo ni la kiupelelezi na haki za mtuhumiwa lipo chini ya Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai (DCI). Tunaendelea na jitihada za kumtafuta DCI Robert Boaz kwaajili ya ufafanuzi zaidi.

Waziri Lugola pia amepiga marufuku tabia ya baadhi ya askari Polisi kutoza fedha kwaajili ya huduma ya dhamana kwa watuhumiwa waliopo mahabusu katika vituo vya polisi nchini.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad