Na Dixon Busagaga
JESHI la Polisi mkoa wa Kilimanjaro kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) wamefanikiwa kukamata kiwanda cha kutengeneza Pombe kali ambacho kimekuwa kikizalisha bidhaa hiyo bila ya usajili.
Moja ya dira za serikali ya awamu ya tano ni kufikia uchumi wa kati kupitia Viwanda ,hata hivyo baadhi ya wafanyabiahara wanatafsiri Dira hii tofauti kwa kuamua kuanzisha Viwanda bila ya kufuata matakwa ya Sheria na taratibu za nchi.
Hali hii imejidhihirisha mkoani Kilimanjaro katika mji mdogo wa Himo baada ya Polisi,TRA na TFDA kubaini uwepo wa kiwanda bandia kinachozalisha Pombe kali .
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ,Kamishna Msaidizi wa Polisi ,Hamisi Issah amesema jeshi la Polisi litaendelea kushirikiana na idara nyingine za serikali kuhakikisha kodi ya serikali inapatikana pamoja na kuhakiki ubora wa bidhaa kwa ajili ya afya ya watumiaji.
Zoezi la kubaini uwepo wa viwanda bandia katka mkoa wa Kilimanjaro ambapo katika siku za karibuni viwanda vilivyogundulika ni vile vinavyotengeneza Pombe za kienyeji na Pombe kali ,baadhi vikiwa katika wilaya ya Rombo.
Mwisho.