Rais Magufuli Aalika Marais wa Nchi Tano Kuja Tanzania

Rais Magufuli aalika Marais wa nchi tano kuja Tanzania
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Mabalozi 5 walioteuliwa kuziwakilisha nchi zao hapa nchini.

Mabalozi waliowasilisha hati zao za utambulisho ni Peter Van Acker РBalozi wa Ubelgiji hapa nchini, Elisabeth Jacobsen РBalozi wa Norway hapa nchini, Anders Sj̦berg РBalozi wa Sweden hapa nchini, Hamdi Abu Ali РBalozi wa Palestina hapa nchini na Mubarak M. Falen Alsehaijan РBalozi wa Kuwait hapa nchini.

Katika mazungumzo na Rais Magufuli baada ya kukabidhi hati zao za utambulisho, Mabalozi hao wameelezea kufurahishwa na uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na nchi hizo na wameahidi kuukuza zaidi hasa katika masuala ya biashara na uwekezaji, teknolojia, utalii na uimarishaji wa huduma za kijamii kwa wananchi.

Rais Magufuli amewapongeza Mabalozi hao kwa kuteuliwa kuziwakilisha nchi zao hapa nchini na amewahakikishia kuwa Tanzania itaendeleza na kukuza zaidi ushirikiano na nchi hizo.

Rais Magufuli amewaomba Mabalozi hao kufikisha shukrani zake kwa viongozi wakuu wa nchi hizo kwa mchango ambao wametoa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo mikopo nafuu ya ujenzi wa miundombinu hasa barabara, umeme, maji, huduma za afya, kilimo na uvuvi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad