Rais Magufuli Ameahidi Kutoa Milioni 20 Kwa Ajili Ya Ujenzi Wa Ofisi Ya Wajasiriamali Wa Eneo La Feri Jijini Dar

Rais Magufuli Ameahidi Kutoa Milioni 20 Kwa Ajili Ya Ujenzi Wa Ofisi Ya Wajasiriamali Wa Eneo La Feri Jijini Dar
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli jana tarehe 1 Oktoba, 2018 ameahidi kutoa shilingi milioni 20 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa ofisi ya wajasiriamali wa eneo la Feri Kivukoni Wilayani Ilala Jijini Dar es Salaam.

Mhe. Rais Magufuli amekutana na Wajasiriamali hao ambao wanajumuisha Wavuvi wadogo na Mamalishe wakati akiwa katika mazoezi ya jioni pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli ambaye pia amewachangia wajasiriamali wanawake shilingi Milioni 5.

Pamoja na kumshukuru Mhe. Rais Magufuli, wajasiriamali hao wameomba awasaidie wasifukuzwe na Manispaa ya Ilala katika eneo hilo, na badala yake wawekewe utaratibu mzuri wa kufanya biashara zao.

Pia wameomba waondolewe ushuru unaotozwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA), kwa mitumbwi ya wavuvi wadogo wa samaki, kama ambavyo Serikali imewaondolea ushuru wakulima wanaopeleka sokoni mazao yasiyozidi tani moja.

Aidha, Wajasiriamali hao wamempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa kazi nzuri ya kuiongoza nchi na kushughulikia kero za Watanzania ikiwa ni pamoja na kuwatembelea na kuwasikiliza kwa mara ya pili.

Kwa upande wake Mhe. Rais Magufuli ameahidi kufanyia kazi maombi ya Wajasiriamali hao na amewapongeza kwa juhudi zao za kujitafutia kipato.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad