Rais Magufuli Aunga Mkono Mgomo wa Minada Zao la Korosho

Rais Magufuli Aunga Mkono Mgomo wa Minada Zao la Korosho
Kufuatia mgomo wa minada ya siku mbili, kwa wakulima wa zao la Korosho mkoani Lindi na Mtwara Rais John Pombe Magufuli, ameeleza kuunga mkono hatua ya maamuzi hayo ya wakulima na kusema yuko nao bega kwa bega.

Maamuzi hayo ya Rais Magufuli yametangazwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa katika kikao na wakuu wa mikoa ya Lindi na Mtwara ambacho kililenga kujadili juu ya hatua ya mgomo wa wakulima wa korosho juu ya kushuka kwa bei ya zao hilo ukilinganisha na miaka 2 iliyopita.

Waziri Mkuu amesema “Rais John Magufuli amewapongeza wakulima wa korosho kwa uamuzi wao wa kukataa kuuza kwa bei ndogo na kueleza yuko pamoja  nao na kumtaka Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba, ajitathimini katika suala la mauzo ya zao la korosho linavyoendelea."

Aidha Waziri Mkuu Majaliwa amesema “haturidhishwi na utendaji wa bodi ya korosho ambao umekiuka maelekezo ya msingi ya Serikali katika kusimamia mfumo mzima wa zao la korosho uliopelekea kuvurugika kwa minada 2.”

Wakulima wa zao hilo katika mikoa ya Lindi na Mtwara walilazimika kuingia kwenye mgomo wa kuuza zao hilo la Korosho kwa kile walichokidai kushuka kwa bei ya zao hilo ukilinganisha na miaka miwili iliyopita huku gharama za uzalishaji zikiwa zimepanda.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad