Rais Trump Kuitoa Marekani Kutoka Mkataba wa Silaha na Urusi

Rais Trump Kuitoa Marekani Kutoka Mkataba wa Silaha na Urusi
Marekani itajitoa kutoka mkataba wa silaha za nyuklia na Urusi, kwa mujibu wa rais Donald Trump.

Akihutubia waandishi wa habari Trump alisema Urusi ilikiuka mkataba wa mwaka 1987 unaofahamika kama Intermediate-Range Nuclear Forces (INF)

Mkataba huo ulipiga marufuku makombora yanayorushwa kutoka ardhini ambayo yanaweza kusafiri umbali wa kati ya kilomita 500 na 5,500.

"Marekani haiwezi kuiruhusu Urusi kuendelea kuunda silaha huku sisi hatuundi," Trump alisema.

Mwaka 2014 Rais Obama aliilaumu Urusi kwa kuvunja makubaliano ya INF baada ya kulifanyia majaribio kombora moja la masafa ya wastani.

Wasiwasi kuhusu hatua ya Urusi ya kuunda makombora yanayokiuka mkataba wa INF ni kitu kinachoighadhabisha serikali ya Trump. Lakini uamuzi wa Trump wa kujitoa ni pigo kubwa katika suala la kudhibiti silaha.

Kiongozi wa Usovieti Mikhail Gorbachev Rais wa Marekani Ronald Reagan walisaini INF mwaka 1987
Wataalamu wengine wanaamini kuwa mazungumzo yangeendelea kujaribu kuleta Urusi kwenye makubaliano.

Marekani inasisitiza kuwa Urusi ilivunja mkataba huo kwa kuunda kombora jipya la masafa ya wastani kwa jina Novator 9M729 - linalofahamika kwa Nato kama SSC-8.

Vifaru vya Urusi vinavyoitia wasiwasi Nato
Linaiwezesha Urusi kufanya shambulizi la nyuklia kwa nchi za Nato kwa onyo fupi sana.

Urusi haijasema chochote kuhusu kombora jipya lakini imekana kuwa ilikiuka makubaliano.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad