MAHAKAMA nchini Korea ya Kusini imemhukumu kifungo cha miaka 15 jela na kumwamru kulipa faini ya dola milioni 11.5 aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Lee Myung-bak (76) baada ya kumtia hatiani kwa makosa ya rushwa.
Lee anakuwa Rais wa nne wa nchi hiyo kuhukumiwa kutumikia kifungo jela baada ya wengine watatu kufungwa kwa makosa ya rushwa.
Mwanasiasa huyo alithibitika kutenda kosa hilo wakati wa uongozi wake baada ya kupokea kiasi cha dola milioni 10 kutoka kwa kampuni ya Samsung na wakati wote wa kesi hiyo, Lee alikuwa akikana mashtaka hayo na kusema kuwa yamechagizwa kisiasa.