Mfumo huo utakuwa ukipokea malalamiko ya watendaji wasiowajibika kuanzia ngazi ya Mitaa, Kata, Wilaya, Mkoa na viongozi Wakuu akiwemo Mkuu wa mkoa,Katibu tawala Mkoa, Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi, Makatibu tawala wilaya na wakuu wa idara Watakuwa wakiona ni mtendaji gani asiewajibika kutatua kero za wananchi.
RC Makonda amesema hataki kuona wananchi wanafika kwenye ofisi za umama na kuambia “Njoo kesho” kila siku pasipokujua kuwa wanatumia nauli na kupoteza muda.
Mfumo utampa mwananchi uwezo wa kueleza malalamiko yake endapo amefika ofisi ya umma na watendaji kushindwa kushughulikia kero zake kwa uzembe.