Ridhiwani Kikwete kuwanunulia kombati jeshi la akiba

Ridhiwani Kikwete kuwanunulia kombati jeshi la akiba
Jeshi la akiba limekuwa ni msaada mkubwa katika jamii ya tanzania kutokana na vijana wengi wanaojiunga na jeshi hilo punde tu wanapomaliza mafunzo hayo upelekea kuwa ni kichocheo kikubwa katika jamii juu ya  suala zima la ulinzi.

Katika jimbo la chalinze mkoani Pwani wahitimu zaidi 400 wanatarajiwa kumaliza mafunzo ya Jeshi la akiba mwezi ujao na hivyo kujifungulia fursa kwa upataji wa ajira kwa vijana hao kupitia kwenye mashirika mbalimbali ya ulinzi katika wilaya hiyo ya Bagamoyo.



Wakizungumza na mbunge wao Ridhiwani Kikwete  vijana walitaja changamoto zinazowakabili kuwa,wengi wao kushindwa kumudu gharama za ununuzi wa kombati mara baada ya mafunzo ya jeshi la akiba kumalizika kutokana na walio wengi kutokuwa na uwezo kiuchumi.

Kurusumu Shabani ni mmoja wa wanamafunzo wa jeshi la akiba alisema kuwa wanampongeza mbunge huyo kwa kuwanunulia wana jeshi la akiba kombati ambazo watazitumia siku ya mwisho ya mafunzo yao.



Aliongeza kuwa ni mafunzo mengi yamefanyika hapa nchini lakini viongozi wachache wenye kuwathamini wahitimu hao kama moja ya sehemu za ulinzi katika jamii, hivyo Kikwete ni kiongozi wa kuigwa katika jamii.

Aidha alisema kuwa vijana walio wengi katika halmashauri ya chalinze wameitikia wito wa kujiunga kwenye jeshi la akiba kutokana na utitili wa viwanda kwenye halmashauri hiyo hivyo ajira za aina nyingi zitapatikana bila wasiwasi kwa kupitia mafunzo hayo.



“Vijana wenzangu onyesheni uzalendo wa dhati katika taifa hili kwa kulitumikia kwa kulinda raia na mali zake pindi mmalizapo mafunzo hayo mkaisaidie jamii katika masuala ya kutokomeza wizi”– Ridhiwani Kikwete.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad