Rufaa ya Mbowe na Wenzake Yatupiliwa Mbali na Mahakama


Rufaa ya Mbowe na Wenzake Yatupiliwa Mbali na Mahakama
Mahakama ya Rufaa imetupilia mbali rufaa iliyofunguliwa na viongozi wa Chadema wakiongozwa na mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe kutokana  na  kasoro za kikanuni katika hati ya taarifa ya kusudio la kukata  rufaa.

Uamuzi  huo wa mahakama ulioandaliwa  na  jopo la majaji watatu wa mahakama hiyo; Dalum Mbarouk (mwenyekiti wa jopo), Shaban Lila na Jacobs Mwambegele, umesomwa  leo Ijumaa Oktoba 5, 2018 na Naibu Msajili, Eddy Fussi.

Kasoro hizo ni hati ya taarifa ya kusudio la kukata rufaa kutobainisha kiini cha uamuzi au amri ya Mahakama Kuu waliokuwa wakiukatia rufaa.

Akisoma uamuzi huo, Fussi amesema kasoro hiyo inaifanya hati hiyo ya taarifa ya kusudio la kukata rufaa kutokuwa na sifa za kuwepo mahakamani, na kwamba kwa hali hiyo mahakama inaitupilia mbali.

Naibu Msajili Fussi amesema kwa kuwa taarifa ya kusudio la kukata rufaa kwenye kesi za jinai ndio msingi wa rufaa, kutupwa kwake kunaifanya hata rufaa yenyewe kukosa uhalali au msingi wa kusimama.

Amefafanua kuwa  haiwezi kusimama yenyewe bila taarifa hiyo ya kusudio la kukata rufaa.

Katika rufaa hiyo, viongozi hao wa Chadema walikuwa wakipinga uamuzi wa Mahakama Kuu uliotolewa na Jaji Rehena Sameji, kutupilia mbali maombi yao ya mapitio ya mwenendo wa kesi yao ya msingi ya jinai inayowakabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Walikuwa wakiiomba Mahakama Kuu iitishe jalada la kesi yao ili kuchunguza na kujiridhisha na uhalali na usahihi wa mwendo wake na amri mbalimbali ambazo mahakama hiyo ilikuwa ikizitoa.

Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kupitia kwa jopo la mawakili wa Serikali, likiongozwa na wakili wa Serikali Mkuu Paul Kadushi aliweka pingamizi, pamoja na mambo mengine akisema kuwa maombi hayo ni batili kwakuwa yanakiuka Sheria ya Mahakama za Hakimu Mkazi.

Mahakama Kuu katika uamuzi wake ilikubaliana na hoja za pingamizi hilo na ikayatupilia mbali maombi hayo ikisema kuwa haina mamlaka ya kuyasikiliza na kutoa amri ambazo vigogo hao wa Chadema walikuwa wakiziomba.

Kutokana na uamuzi huo ndipo walipokata rufaa Mahakama ya Rufani
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad