Rungwe amkana diwani wa CCM, aeleza kila kitu


Mwenyekiti wa Chama Cha Ukombozi (CHAUMA) Hashim Rungwe amezungumzia taarifa zilizozagaa za kupokea diwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Makongo ambaye anatajwa kujiunga na chama chake mapema wiki hii.

Kupitia mitandao ya kijamii kulisambaa taarifa juu ya kuwepo kwa diwani wa kata ya Makongo jijini Dar es salaam aliyefahamika kwa jina la Mark Mwinshaha, ambaye ilielezwa amehama CCM bila kutajwa kwa sababu yeyote.

Hashim Rungwe amesema hajapokea diwani yeyote kutoka kwa Chama Cha Mapinduzi.

Hivi karibuni kumekuwa na wimbi kubwa la wanasiasa wa upinzani nchini kuhama vyama vyao na kuhamia CCM kwa ajili ya kuunga mkono jitihada za Rais Dkt John Pombe Magufuli.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad