Sababu ya Samatta kuwa kivutio klabu za England yabainika


Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayechezea klabu ya KRC Genk, Mbwana  Samatta anang'ang'aniwa na klabu tatu za England, taarifa za vyombo vya habari nchini Uingereza zinasema. 

Tetesi zinasema nyota huyo anatafutwa na West Ham United, Everton na Burnley. 
Samatta, 25, maarufu kwa Watanzania kama 'Samagoal' ameng'aa sana akichezea klabu ya KRC Genk nchini Ubelgiji. 

Amefungia klabu hiyo mabao 11 katika mechi 16 ambazo amechezea msimu huu, nusu ya mabao hayo akiyafunga barani Ulaya. 

Taarifa za kumhusisha Samatta na klabu ya Everton zimetoka kwa mtandao wa hitc.com, mmoja wa mitandao ambayo imeibukia kuwa maarufu kwa taarifa za wachezaji na kuhama kwao. 

Samatta, mwenye kimo cha futi 5 inchi 11, amefunga mabao sita katika ligi ndogo ya klabu barani Ulaya, Europa League, na ni hapo ameanza kuonekana na klabu za England. 

Mnamo 23 Agosti 2018 Samatta, alifunga 'hat-trick' dhidi ya Brøndby IF katika Europa League kwenye mechi ambayo walishinda 5-2. 

Everton wametatizika kumpata mshambuliaji wa kutegemewa tangu nyota wao Romelu Lukaku alipowaacha na kuhamia Manchester United kwa £75 mwaka 2017. 
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad