Sakata la Mabasi ya Mwendokasi Lamuibua RC Makonda "Watendaji Wote Niwakute Kimara Kesho Saa 12:30 Asubuhi"


Sakata la Mabasi ya Mwendokasi Lamuibua RC Makonda "Watendaji Wote Niwakute Kimara Kesho Saa 12:30 Asubuhi"
Tatizo linalowapata wakazi wa Dar kupitia mradi wa mwendokasi limemuibua mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mh. Poul Makonda na kuonyesha Hisia zake za kukerwa na uendeshaji wa mradi wa mabasi hayo na kuagiza watendaji wote wanaosimamia mradi huo kukutana naye kesho saa 12:30 asubuhi katika kituo cha mabasi hayo kimara.

Kauli hiyo ya mkuu wa mkoa ameitoa katika ukurasa wake wa instaramu na kuandika hivi;

Sifurahishwi na namna mradi wa mwendokasi unavyoendeshwa kwani matarajio ya Mh. Rais ni kuona changamoto ya muda mrefu ya usafiri Kwa wananchi wa jiji la Dar es Salaam ikigeuzwa historia kupitia mradi huu. Kwasababu hizo nimeagiza watendaji wote wanaosimamia mwendokasi niwakute Kimara stand ya mwendokasi kesho Saa 12:30 asubuhi wanieleze kwanini hakuna hatua madhubuti walizochukua huku wakishuhudia kero wanazopitia wananchi.
Nitumie pia fursa hii kuwaomba radhi wananchi Kwa kero hii na niwaahidi kuwa jambo hili litapatiwa ufumbuzi hivi karibuni. Tukutane mapema asubuhi mwendokasi kimara.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad