Ujerumani, Ufaransa na Uingereza kwa pamoja zimetoa wito zikitaka uchunguzi wa kina ufanyike kuhusiana na kutoweka kwa Jamal Khashoggi hiyo ikiwa ni kwa mibu wa taarifa iliyosainiwa na waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Jeremy Hunt , Jean-Yves Le Drian wa Ufaransa na waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Heiko Maas.
Ufalme wa Saudi Arabia unasema tuhuma dhidi yake kuhusiana na suala la Khashoggi hazina msingi. Hata hivyo ufalme huo haujatoa ushahidi unao onesha mwandishi huyo wa habari ambaye amekuwa akimkosoa mfalme wa Saudia Mohammed bin Salman kama aliondoka katika ubalozi wa mdogo wa Saudi Arabia mjini Istanbul.
Kwa upande mwingine Trump amesema Marekani itakuwa inajiadhibu yenyewe iwapo itasitisha mauzo ya silaha kwa Saudi Arabia kwani silaha hizo zinauzwa na makampuni ya Marekani na hata kama Saudi Arabia haitanunua silaha kutoka makampuni ya Marekani basi itanunua kwingine.
Khashogi anayeandikia pia gazeti la Washington Post alitoweka Oktoba 2 baada ya kuingia ubalozi mdogo wa Saudi Arabia mjini Istanbul.
Tayari viongozi wa kimataifa wanaohusika na masuala ya kibiashara wameanza kujiondoa kushiriki kongamano lijalo la uwekezaji katika taifa hilo la kifalme lililopewa jina la “kongamano la Davos jangwani”
Hayo yanajiri mnamo wakati biashara ya kubadilisha fedha ikiporomoka hadi kufikia kiwango cha alama zaidi ya 500 kabla ya kufikia alama 264 au baadaye kufikia zaidi ya asilimia 4.
Issam Kassabieh mchambuzi wa masuala ya fedha katika kampuni moja ya masuala ya fedha iliyo na makao yake mjini Dubai anasema suala kama hili lazima litaogopesha wawekezaji kwani hawaoni kama wako salama nchini Saudi Arabia kwa hiyo ni rahisi kuondoa uwekezaji wao.
Ikulu ya Marekani imepuuza vitisho vya Saudi Arabia kwamba huenda ikalipiza kisasi kwa hatua yoyote ya Marekani kuiadhibu kichumi falme hiyo, kuhusiana na tuhuma za mauaji ya mwandishi Khashoggi, huku ikitoa wito wa uchunguzi ulio wazi kuhusiana na kutoweka kwake.
Maseneta wawili wa chama cha Republican, wamesema bunge la Marekani liko tayari kuchukua hatua ikiwa ni pamoja na uwezekano wa kuzuwia uauzaji silaha kwa Saudi Arabia.
Mshauri wa masuala sya uchumi wa Ikulu ya White house Larry Kudlow alikataa kutabiri kile kitakachofanywa na Rais Donald Trump baada ya kuahidi hatua kali wakati wa mahojiano ya dakika 60 hapa Jumapili, ikiwa Marekani itakuwa na ushahidi kwamba Khashoggi aliuwawa ndani ya ubalozi mdogo wa Saudi Arabia mjini Istanbul.
Akizungumza katika mahojiano yaliyoendeshwa na kituo cha matangazo cha CBS rais Donald Trump alisema Marekani italifuatilia kwa kina suala hilo na kutakuwa na adhabu kali kwa anayehusika.
Chanzo Dw Swahili.