Samatta Basi Tena Hakamatiki Atupia Europa League na Kuweka Rekodi Hii

Samatta Basi Tena Hakamatiki Aweka Rekodi Hii
Mshambuliaji wa klabu ya Genk ambaye ni nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', Mbwana Samatta ameendeleza moto wa kupachika mabao katika michuano ya 'Europa League' usiku wa jana.


Samatta amepachika mabao mawili na kuisaidia Genk kuondoka na alama tatu kwa kuichapa Besiktas mabao 4-2 katika uwanja wake wa nyumbani mjini Instanbul, Uturuki.

Samatta alifunga mabao yake dakika za 23 na 69, akimfunga mlinda mlango, Loris Karius aliyejiunga Besiktas kwa mkopo akitokea  Liverpool msimu huu. Karius alisimama langoni mwa Liverpool katika fainali ya klabu bingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid mwezi Mei mwaka huu, fainali ambayo Liverpool ilichapwa mabao 3-1.

Mabao mengine ya Genk katika mchezo huo usiku wa jana yalifungwa na viungo Dieumerci N'Dongala kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) dakika ya 81 na Jakub Piotrowski dakika ya 83, huku mabao ya Besiktas yalifungwa na Vágner Love katika dakika ya 74 na 86 ya mchezo.

Genk sasa inaongoza kundi I baada ya kufikisha pointi sita kufuatia kucheza mechi tatu, ikishinda mbili na kufungwa moja, inafuatiwa na Malmo FF yenye pointi nne sawa na Sarpsborg 08, wakati Besiktas yenye pointi tatu inashika mkia.

Samatta jana amefikisha mechi 124 katika mashindano yote tangu amejiunga na Genk Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Congo (DRC) na amefunga jumla ya mabao 47. Katika Ligi ya Ubelgiji amecheza mechi 96 na kufunga mabao 33, Kombe la Ubelgiji mechi nane mabao mawili na Europa League mechi 20 mabao 14.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad