Mchezaji mkongwe wa Cameroon, Samuel Eto’o Fils leo anakutana na Rais mstaafu wa awamu ya nne, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete ofsini kwake Masaki jijini Dar es Salaam kabla ya kuanza safari kurudi Nchini Doha, QATAR.
Eto’o amefurahi sana kukutana na Rais Mstaafu na kusalimiana nae pamoja na kupiga picha nae ambayo kwake amesema amepawa hadhi ambayo hakuitefemea.
Eto’o akiwa anaanza safari yake kuna Tanzania katika moja ya watu aliopenda kuonana nao ni Rais Jakaya Mrisho Kikwete ambaye alimfahamu toka enzi hizo miongoni mwa Marais ni Rais pekee anayependa michezo na wanamichezo kwa ujumla.
Eto’o alifurahi sana waliofanya juhudi za kumkutanisha na Rais mstaafu pamoja na kuwa ni dakika za mwisho akielekea Airport lakini alisema hakika ameimaliza ziara yake kwa Furaha ya kukutana na mtu muhimu sana katika maisha yake.
Eto’o alikuwa Nchini kwa uzinduzi wa Uwanja wa Mpira wa Miguu wa wachezaji Watano watano ujulikanao kama 5s(5 – aside) ukiofanyika juzi Jumatano 11octoba 2018 maeneo ya Coco Beach karibu na jengo la Coco Plaza Ostarbay jijini Dar es Salaam.