Saudi Arabia Yatakiwa Kutoa Maelezo ya Kina Mauaji ya Mwanahabari

Saudi Arabia yatakiwa kutoa maelezo ya kina mauaji ya mwanahabari
Nchi tatu zenye ushawishi mkubwa barani Ulaya, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani zimelaani vikali mauaji ya mwandishi Jamal Khashoggi na kuitaka Saudi Arabia kutoa ufafanuzi wa kina haraka iwezekanavyo.

Taarifa ya pamoja ya mataifa hayo yanaitaka Saudia kutoa vielelezo vya kina juu ya madai kuwa Khashoggi aliuawa wakati akijaribu kupigana ndani ya ofisi za ubalozi mdogo wa Saudia jijini Istanbul, Uturuki.

Rais wa Marekani Donald Trump pia amebainisha kuwa "hakuridhishwa" na maelezo hayo ya Saudia.

Saudia yasema Khashoggi alifariki alipojaribu kupigana, Uturuki yaapa kufichua yaliotokea
Khashoggi azidi kuumiza vichwa
UN yaingilia kati kutoweka kwa Jamal Khashoggi
Rais wa Uturuki Racep Tayyip Erdogan jana Jumapili ameahidi kudhihirisha ukweli wote juu ya tukio hilo.

Erdogan amesema atatoa maelezo juu ya sakata hilo kesho Jumanne atakapolihutubia bunge la nchi hiyo.

"Tunataka haki itendeke hapa, na juu ya jambo hili tutadhihirisha ukweli wote," Erdogan aliuambia mkutano wa hadhara jijini Istanbul.

Khashoggi aliingia katika jingo la ubalozi mdogo mnamo tarehe 2 Oktoba kwa minajili ya kushughulikia karatasi zake muhimu kuhusiana masuala ya ndoa.

Awali mamlaka za Saudia zilidai kuwa alitoka, lakini mamlaka za Uturuki zilikanusha vikali na kusema kuwa wanaushahidi kuwa mwanahabari huyo alizuiliwa na baadae kuuawa na kisha mwili wake kukatwa vipande vipande.

Uturuki: Mwandishi 'aliuawa' ndani ya ubalozi wa Saudi Arabia

Khashoggi alikuwa mkosoaji kinara wa sera za Mwanamfalme Mohammed Bin Salman na alihamia Marekani mwaka 2017 akihofia usalama wake.

Katika taarifa yao ya pamoja, nchi za Uingereza, Ufaransa na Ujerumani zimesema kuwa zimeshtushwa na mkasa huo wakiamini hakuna sababu yeyote ile ya kutetea mauaji.

"Maelezo Zaidi na yenye ushahidi usiokuwa na chembe ya shaka yanahitajika… Hivyo basi, tunataka uchunguzi wa kina ufanyike na wahusika wote watambulike na hatua za kisheria zinastohili zichukuliwe kwa waliotenda unyama huu."

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad