Serikali Walikumbuka Daraja la Manzese Lapakwa Rangi

Serikali Walikumbuka Daraja la Manzese Lapakwa Rangi
Ukizungumzia taswira ya jiji la Dar es Salaam huwezi kuliacha Daraja la Manzese. Miaka kadhaa iliyopita Daraja la Manzese ndio lilibeba umaarufu wa Dar es Salaam ambapo watu mbalimbali ndani na nje ya jiji hilo walikuwa wakifika maeneo hayo kama sehemu ya utalii.

Katika kipindi hicho Daraja hilo ndilo lilikuwa daraja pekee Dar es Salaam linalomuwezesha mtu kutoka upande mmoja wa barabara hadi upande mwingine.

Historia ya Daraja hili haiwezi kufutika kwa sababu watu wa hali ya Chini wamekuwa wakifika hapo kama sehemu ya Kiutalii, kupiga picha na wengine kupiga soga.

Pia katika historia unaambiwa Daraja la Manzese ndio lilikuwa kama Kituo kikuu cha Dar es Salaam ambapo mgeni akitokea mkoani lazima asubiri katika eneo hilo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad