Serikali ya Tanzania Yazikataa Msaada wa Dola 50 milionKutoka Benki ya Dunia

Serikali ya Tanzania yazikataa Dola 50 milioni za msaada kutoka Benki ya Dunia
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James amesema hawatambui msaada wa Dola 50 milioni ambazo zinadaiwa zimesitishwa na Benki ya Dunia (WB).


“Serikali haijawahi kuomba wala kuwa kwenye mchakato wa kukopa Dola 50 milioni kwenda kwenye kazi za Ofisi ya Taifa ya Takwimu. Mimi kama Katibu Mkuu nasema hatujawahi kuandika barua kuomba hizo fedha,” amesema James alipozungumza na MCL Digital leo jioni Oktoba 2, 2018.

Licha ya maoni hayo, katibu mkuu huyo ameitaka MCL Digital kuzungumza na mkurugenzi mkazi wa WB, Bella Bird kujiridhisha kuhusu maombi ya fedha hizo huku akikiri kuwepo kwa mikopo mingine kutoka benki hiyo inayoendelea kutolewa.

Hata hivyo alipotafutwa msemaji wa benki hiyo, Loy Nabeta amesema majibu yaliyotolewa na benki hiyo yalikuwa yanafafanua hoja za mtandao uliochapisha habari husika.

“Majibu yametoka makao makuu (New York-Marekani). Hatuna cha kuongeza wala kupunguza,” amesema

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad