Hili limethibitika ikiwa ni takribani wiki tatu tangu vituo hivyo vya Afya visimamishe kutoa huduma nchini
Afisa uhusiano wa Marie Stopes, Dotto Mnyadi amesema huduma zimesimamishwa kutokana na ukaguzi uliokuwa ukifanywa na Serikali pamoja na ukarabati
Hata hivyo, Naibu Waziri wa TAMISEMI anayehusika na Masuala ya Afya, Josephat Kandege jana alisema Marie Stopes imesitishiwa kutokana na kukiuka miongozo
Vituo vinavyoelezwa kufungiwa vipo Arusha, Mwanza, Musoma, Iringa, Mbeya, Kahama, Temeke, Kimara, Mabibo na Hospitali ya Mwenge isipokuwa kituo cha Zanzibar