Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Shilole Alhamisi hii amelamba deal nono la ubalozi wa bidhaa mpya kutoka CRDB iitwayo, Sim Account. Kwa sasa watumiaji mbalimbali wa huduma hiyo ya ‘Sim Account’ ya wanajishindia mamilioni ya pesa kupitia promotion mpya ya ‘Shinda na Sim Account’.
Akiongea na Bongo5 muda mchache ya kulamba deal hilo, Shishi alisema anawashukuru CRDB kwa kuona anafaa kuiwakilisha brand hiyo huku akidai wateja wake wa ‘Shishi Trump Food’ watalipa kiurahisi kupitia huduma hiyo ya Sim Account.
“Nimefurahi sana kuwa balozi wa Sim Account kwa sababu ni huduma ambayo anaona kabisa inaenda kurahisisha maisha wa watu wa chini, wanavikoba wenzangu, ukitaka kulipa kitu ni rahisi sana na ni huduma ambayo hata mimi mwenyewe nikikaa mbele ya watu wanaweza kujivunia nayo. Kwahiyo nimeaambie tu Watanzania wenzangu na mashabiki wa Shishi, huu ni muda wa kuanza kwenda kidigitali zaidi,” alisema Shilole.
Aliongeza,”Kwenye biashara yangu ya Shishi Trump Food wateja hawatapata tabu kabisa, ishu za chenji zilikuwa zinasumbua sana lakini sasa hivi kwa Sim Account unaweza kulipa kile unachodaiwa bila usumbufu wa chenji. Pia Sim Account inahuduma mbalimbali ndani yake kama zakulipa bili, wale wenzangu wa vikoba, yaani ni kitu ambacho ukiwa nacho hautapata tabu kabisa kwenye ishu za manunuzi,”
Mapema leo baada ya muimbaji huyo tutangazwa kuwa balozi, CRDB walitangaza majina ya washindi katika droo ya leo ya shinda na Simaccount ambapo bwana Lukas Kihulu kutoka Mkaranga mkoani Ruvuma aliibuka na milioni 2 huku mshindi wa pili akiwa ni Jamal Twahir kutoka Milidu Mtwara ambaye aliibuka na milioni 1.
Zawadi zinazoshindaniwa ni milioni 25 kwa kila mwezi, milioni 5 kwa kila wiki na milioni 1 kwa kila siku. Unachotakiwa kufanya ni kupiga *150*62# ili ujiunge na wewe uanze kushinda zawadi mbalimbali.
Related Articles
Shilole Apata Shavu CRDB Apewa Ubalozi wa Sim Account
0
October 04, 2018
Tags